Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi kwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Morogoro (RCO)
kufuatia unyanyaswaji unaofanywa kwa wamiliki wa Kiwanda Cha Tumbaku Mjini humo.
Rais Magufuli alitoa agizo hilo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani kwenye mkutano wake na wafanya biashara Jijini Dar es Salaam kufuatia
kufuatia malalamiko yaliyotolewa na muwakilishi wa wafanyabiashara wa mkoa wa morogoro ndugu Paschal Kihanga.
Kihanga alisema, Kiwanda cha Tumbaku Morogoro (TLTC) kina wafanyakazi zaidi ya 2600 lakini kimeshaanza kupunguza idadi ya wafanyakazi na kinaelekea kufungwa kabisa kutokana na kusumbuliwa na Polisi na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Amesema, Polisi wanawasumbua wamiliki wa kiwanda hicho, wanawakamata na kuwaweka ndani bila sababu za msingi na bila kuwafungulia mashitaka Aliongeza kuwa Tatizo lililopo walishaliripoti kwa mkuu wa mkoa na kujibiwa kuwa amesharipoti kwenye Wizara husika
Rais Magufuli alipohoji ni nini hasa tatizo linalopelekea wakamatwe, Kihanga alijibu tatizo wanaloripotiwa nalo ni mrundikano wa kodi lakini hawakuwahi kuwafunguliwa mashtaka yeyote zaidi ya kuwaeka ndani tu. Rais Magufuli alipoomba ufafanuzi, Waziri wa Uwekezaji Anjela Kairuki alisema, alishafanya kikao na kiwanda hicho, na walishakaa kikao kingine na mawaziri wa fedha, kilimo, naibu mwanasheria mkuu wa serikali na wengine na alishamuandikia barua waziri wa mambo ya ndani juu ya suala hilo. “Waziri wa Mambo ya Ndani alishafanya ziara kiwandani na kuna maelezo ambayo ameyatoa na lipo jalada pia ambalo amelielekeza na linatafutwa, naamini baada ya hapo kuna maelekezo ambayo waziri wa mambo ya ndani atayatoa.
Alipoulizwa na Mh. Rais kuhusu nini hasa tatizo Kairuki alisema, tatizo ni baadhi ya wakurugenzi, hasa wazawa, walifunguliwa mashitaka lakini walivyolazwa ndani na polisi baada ya muda fulani hawakuwahi kupelekwa mahakamani na wala hawakuambiwa makosa yao ni yapi. “Baada ya muda kupita na kulalamika katika vyombo mbalimbali wakatolewa, kwa hiyo walivyokuja kulalamika kwetu ndio tukafikisha kwa Waziri wa mambo ya ndani ambaye alishawatembelea ili apewe maelekezo zaidi juu ya nini hasa tatizo lililopelekea kulazwa ndani,” alisema Kairuki Rais Magufuli alipomuhoji Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Meja Jenerali Jacob Kingu juu ya taarifa hizo alisema suala hilo kweli lilifika wizara ya mambo ya ndani ya nchi na walishatembelea kiwanda hicho na kuongea na viongozi. Aliongeza kuwa, suala hilo limefanyiwa kazi na wale wote waliohusika kwa upande wa polisi wamechukuliwa hatua.
Raisi Magufuli alipohoji ni hatua gani zilizochukuliwa alijibiwa kuwa RPC wa Morogoro ameshawafungulia mashtaka wale wote waliokiuka taratibu za kuwaeka ndani wamiliki wa kiwanda cha Tumbaku na wote walioonekana kuchukua rushwa Kufuatia maelezo hayo, Rais Magufuli alitoa maagizo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani kuwa muhusika asimamishwe kazi na apelekwe mahakamani. Amesema kama RCO ndio anayehusika, asimamishwe na apelekwe mahakamani ambapo Jenerali Kingu aliitikia amri hiyo. Rais Magufuli aliendelea kwa kumuhoji Afisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ikiwa kama amelifuatilia suala la rushwa linaloendelea katika kiwanda hicho na kujibiwa kuwa, hana taarifa za rushwa dhidi ya kampuni hiyo na kuahidi kuifuatilia taarifa hiyo na kuifanyia kazi haraka iwezekanavyo. Rais Magufuli aliagiza taarifa hiyo ipatikane haraka iwezekanavyo ili suluhu ya kweli ipatikane na watu wasiwe wamesingiziwa. Mbali na sakata hilo, RAis Magufuli alishangazwa na kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kushindwa kushughulikia tatizo hilo licha ya kuwa yeye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa.
Raisi magufuli alishangazwa na kitendo cha polisi kufanya unyanyasaji huku mkuu wa mkoa anatazamaRais Magufuli alisema ikiwa kiwanda kitafungwa na watu wote kuacha kazi, serikali haitaweza kukusanya mapato. Alisema, hata hiyo mishahara wanayolipwa mapolisi inatokana na mapato hayo
|
No comments