LIVERPOOL|| Je shinikizo la kushinda taji la ligi kuu England linamshinda Jurgen Klopp?|SportsUPDATES.
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp kwa mara nyingi huwa ni mwingi wa bashasha na tabasamu - lakini sasa Je anakabiliwa na shinikizo kwa kutetereka kwa timu yake katika mpambano wa kulinyanyua taji katika ligi kuu England?
Timu hiyo imekuwa juu na kwa pointi saba mbele dhidi ya mabingwa Manchester City, ambao walikuwa wa pili walipokuwa wakielekea kwenye mechi Januari 3.City ilishinda 2-1 na miezi miwili baadaye leo, Liverpool imeshuka kwa pointi moja nyuma ya wapinzani wao kufuatia mechi 8 za ligi nne kati yazo zikiishia kwa sare.
Timu ya Klopp ilikabiliwa na uhaba wa magoli dhidi ya wapinzani wao katika mechi ya derby iliyopita, na kulikuwa na ishara baada ya mechi kwamba shinikizo linamzidi Meneja huyo raia wa Ujerumani.
Klopp ajibizana na muokota mpira Goodison Park.
Kufuatia mechi ya Jumapili huko Goodison Park, Klopp hakuwa na furaha alipomfuata muokota mpira ambaye kwa kejeli alimpigia makofi alipokuwa akitoka uwanjani.
Klopp aliondoka akitabasamu baada ya kujibizana kwa kifupi, lakini alikasirishwa na mwandishi habari ambaye baadaye aliyemuuliza swali kuhusu mtazamo wa timu yake dhidi ya Everton wakati wa mkutano na waandishi habari baada ya mechi.
No comments