ETO'O ASHITAKIWA KWA KUTELEKEZA WATOTO|FacksonMEDIA
Neves anasema wakati Eto’o akiwa anachezea Leganes alizaa nae mtoto ambaye kwa sasa ana miaka 19.
Lakini Eto’o hakuwahi kumtambua mtoto huyo anayejulikana kama Erika.
mwanasheria wa mwana mama huyo amesema tayari kesi imeshafunguliwa jijini Madrid na itasikilizwa tarehe 24 mwezi April mwaka huu.
Mwanamama huyo amedai kuwa walianza mahusiano yao ya siri na Eto’o mwaka 1997 wakati Eto’o akiwa anacheza kwa mkopo ndani ha klabu ya Leganes akitokea Madrid.
Neves ni mzaliwa wa Cape Verde anadai baadae aligundua kuwa yeye ni mjamzito ambapo alijifungua mwaka 1999.
Mahakama itaamuru vipimo vya DNA kufanyika ili kujua ukweli wa suala hilo.
No comments