RECENT UPDATES

SPORTS | Mvulana wa Kenya apewa jezi na nyota wa Arsenal baada ya picha yake kusambaa mitandaoni|FacksonMEDIA.


 Picha ya kijana mdogo akichunga ng'ombe akiwa amevaa jezi au fulana
aliyoiandika jina la Mesut Ozil na chapa ya number ya mchezaji huyo imewavutia wengi katika mitandao ya kijamii akiwemo nyota mwenyewe wa soka.
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Arsenal Mesut Ozil amemnyooshea mkono mvulana mdogo kutoka nchini Kenya, Lawrence ambaye picha yake akiwa amevaa jezi bandia ilitumwa katika ujumbe wa twitter kwenye akaunti ya Ozil mwaka jana.
Picha ya Lawrence akiwa amevaa jezi halisi iliyotiwa saini na nyota huyo, mojawapo kati ya tano alizotumiwa kama zawadi, imesambazwa katika mitandao ya kijamii na kupendwa na kupongezwa na wengi.

Akizungumza na BBC, Eric Njiru mwandishi nchini Kenya aliyempiga picha mvulana huyo mwaka jana, anasema anahisi furaha sana kwa kuwa amefanikiwa kumuunganisha mchezaji wa kimataifa, wa timu ya taifa Ujerumani, aliyeshinda kombe la dunia, na kijana ambaye anatoka maeneo ya Nairobi.
'Sio watu wengi wanaoweza kupata fursa ya kuongea na mchezaji wa Uingereza, wacha hata ligu ya juu, hata kwa ligi za chini, sisi wenyewe wakenya hatujapata fursa ya kuongea na mchezaji kama Origi ambaye babake ni Mkenya', amesema Njiru akielezea fursa hiyo adimu.
Ameeleza huenda Lawrence ni mdogo kwa sasa kutambua thamani ya fursa hiyo lakini anaamini akiwa mkubwa na akitazama nyuma, atatambua ukubwa wa hatua hiyo.
Njiru aliituma picha hiyo mwishoni mwa mwaka jana kama ujumbe kwenye akaunti ya twitter ya Ozil
Njiru ambaye binafsi ni shabiki wa timu hasimu ya Liverpool katika ligi ya Uingereza anasema hakutarajia kupata jibu kutoka kwa Ozil alipotuma ujumbe huo mara ya kwanza mwaka jana.
'Huyu kijana nilimuona, nikajiona mimi nilikuwa hivi nikiwa mdogo, yaani alinifurahisha sana, kumuona aliandika shati lake Ozil nyuma kwa kalamu, na nikatamani sana apate shati halisi kutoka kwa Ozil siku moja'.

Lakini kijana Lawrence amepokeaje zawadi kutoka kwa Ozil?

Alifurahi sana, na sio tu siku ya kupokea zawadi hiyo.
Njiru anaeleza kwamba kuanzia siku alipomueleza kwamba Ozil alijibu ujumbe aliotuma na kwamba mchezaji huyo angependa kujua kumhusu, anakoishi, anakosoma, alifurahi sana pamoja na familia yake nzima.
'Hakuamini ila siku tulipofika kupeleka zawadi ya mashati hayo, ndipo alishtuka yaani mumekuja? kumbe ni kweli? hakuamini kabisa.

Je Lawrence atakutana na Mesut Ozil?

Njiru ameeleza kwamba mawasiliano yameidhinishwa na kwamba amemtumia Ozil ujumbe wa video kutoka kwa Lawrnce akisema kwamba angependa kuonana na Ozil.
Inatarajiwa kwamba Ozil ataiweka video ya ujumbe wake Lawrence leo katika ukurasa wake.
Hatahivyo uamuzi wa mwisho Njiru anasema utakuwa wa mchezaji huyo nyota wa Arsenal.
Nyota huyo wa soka amejizolea sifa kede kede kutoka kwa watu waliomiminika kujibu ujumbe kwenye Twitter ambao umesambazwa kwa zaidi ya laki moja na nusu, wengi wakimpongeza kwa ukarimu wake hata kwa wasio mashabiki wa timu ya Arsenali anayoichezea nyota huyo:
Hadithi ya Lawrence kutoka Kenya inawiana na ile ya mvulana wa Afghanistan ambaye aligonga vichwa vya mitandao ya kijamii alipovaa fulana ya mfuko wa plastiki ilio na jina la Lionel Messi hatimaye amepata jezi nzuri kutoka kwa mshambuliaji huyo wa Argentina.
BBC ilimsaidia Messi kumtafuta mtoto huyo ambaye anajulikana kuwa shabiki mkubwa wa mchezaji huyo wa Argentina.
Murtaza Ahmadi mwenye umri wa miaka 5, anatoka katika wilaya ya Jaghori mashariki mwa mkoa wa Ghazni nchini Afghanistan.
Haki miliki ya picha TWITTER JOYNAW5
Image caption Murtaza Ahmadi wa miaka 5 alitumiwa jezi ya Messi iliotiwa saini baada ya picha yake hii kusambaa
Timu ya usimamizi wa Messi ilithibitisha kwamba Murtaza alitumiwa jezi ya mshambuliaji huyo wa Argentina iliotiwa saini pamoja na mpira kutoka kwa mshambuliaji huyo wa Barcelona ambaye ametuzwa kuwa mchezaji bora mara tano.
aisha?

No comments