RECENT UPDATES

FacksonMEDIA |Jack Grealish ashambuliwa na shabiki katika game ya Birmingham na Aston Villa|NewUPDATES.

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Aston Villa Jack Grealish ameshambuliwa na shabiki aliyekimbilia uwanjani katika mechi ya Aston Villa dhidi ya mahasimu wao Birmingham Villa Jumapili.
Shambulio hilo lilitokea katika takika ya 10 wakati mwanamume aliyekuwa amevalia kofia alipojitosa uwanjani na kupita nyuma yake kabla ya kupitisha mkono wake hadi kwenye uso wa Grealish.
Ethiopian Airlines: Uraia wa abiria waliokufa watambuliwa
Shabiki huyo ambaye alikuwa amevalia jaketi ya Birmingham City, alibusu mikono yake huku akiashiria kutuma busu zake kwa umati wa mashabiki alipokua akiondoshwa uwanjani .
Polisi wa kituo cha West midlands wamesema mwanamume huyo amelkamatwa kufuatia tukio hilo.
Wageni walishinda mchezo huo kwa 1-0, huku Grealish akipata bao la ushindi mnamo dakika ya 67 ya mchezo.
Shirikisho la soka la England EFL limetoa taarifa likilaani kitendo cha mwnamume huyo , na kuongeza kuwa : "Ni hali ambayo mchezaji yeyote hapaswi kukabiliana nayo .
"Wale wanaocheza katika mechi wanapaswa kucheza wakiwa hawategemei kukabilian ana hali kama hii.
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Grealish aliketi chini uwanjani wakati shabiki mwanamume alipomvamia
Birmingham iliomba radhi kwa Grealish na Villamara moja baada ya mechi na kuongeza kuwa watachunguza upya usalama wa uwanja wao.
"Tunalaani tabia ya mtu binafsi ambaye alifanya kitendo hiki na tutahakikisha kuwa anapigwa marufuku kuingia St Andrew's kwa maisha yake yote," ilisema taarifa ya the Blues.
"Klabu pia itaunga mkono adhabu zaidi zitakazotolewa kwa muhusika kulingana na sheria.

No comments